Takriban watu 15 wamefariki dunia na wengine 29 kujeruhiwa ambapo 7 kati yao wapo katika hali mbaya baada ya kutokea kwa ajali ya barabarani eneo la Daraja pacha kando ya Barabara kuu ya Nakuru kuelekea Eldoret, Nchini Kenya.

Taarifa ya Polisi kitengo cha Usalama Barabarani imeeleza kuwa ajali hiyo iliyotokea Januari 9, 2024 asubuhi ikihusisha Basi la Classic Kings of Congo na Matatu ya North Ways huku Afisa wa Huduma ya Kitaifa ya Polisi – NPS, akisema maafisa wake kutoka Kituo cha Polisi cha Mau Summit walifika kwa wakati eneo la tukio.

Waliojeruhiwa walikimbizwa katika Hospitali ya Kaunti Ndogo ya Molo na Mkuu wa polisi wa Kuresoi Kaskazini, Judah Gathenge alisema abiria wote waliokuwa kwenye matatu hiyo iliyokuwa ikielekea Nairobi, walipoteza maisha.

Basi hilo lilikuwa likisafiri kutoka Nairobi kwenda Kampala, Uganda na waliofariki ni watu wazima wanane na watoto saba, kati yao wasichana watano na wavulana wawili.

Mchengerwa amkabidhi Mhagama Mil. 20
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Januari 10, 2024