Mshukiwa mkuu wa mauaji ya Shakahola, Mchungaji Paul Mackenzie amesema yupo tayari kufa kuliko kuendelea kuteseka gerezani, akidai anapitia wakati mgumu kwa kunyimwa huduma muhimu za malazi na chakula.

Mackenzie ameyasema hayo mwishoni mwa wiki iliyopita huko Shanzu akidai anapitia mateso Gerezani, ikiwemo kufungiwa kwenye chumba chenye giza siku mbili bila kupewa chakula wala kupata nafasi ya kuoga.

Mbele ya Hakimu Mkuu Mwandamizi, Yusuf Shikanda alisema majaribio yake ya kutafuta usaidizi kutoka kwa wakubwa wa Gereza hayajazaa matunda na hivyo ni bora afe kuliko kuteseka kwani ni wazi wasimamizi wakuu katika gereza hilo wanaonekana kupanga kumdhulumu haki.

“Mimi na wenzangu tumefanya uamuzi. Ukiona umenichoka mimi na wenzangu, tuko tayari kupelekwa Mto Yala. Hatuna shida na hilo kwa sababu nitakufa, na wewe kiongozi wa mashtaka siku moja utakufa kama mimi. Hakuna mahali utajificha,” alisema Mackenzie na kuongeza kuwa hajafungua kanisa lolote ndani ya gereza hilo alisema Mackenzie.

Vijana wamekosa mwelekeo - ACT-Wazalendo
Gamondi achekelea Young Africans