Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mohamed Mchengerwa amekabidhi Sh. Milioni 20 kwa Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Jenista Mhagama kutoka kwa Umoja wa Maafisa Elimu wa Mkoa na Halmashauri zote nchini kwa ajili ya waathirika wa mafuriko ya Hanang mkoani Manyara.

Fedha hizo zimekabidhiwa kwa Waziri Jenista katika Ofisi yake ndogo, Jijini Dar es salaam, ambapo amepokea fedha hizo kwa niaba ya Ofisi ya Waziri Mkuu, huku Mchengerwa akisema fedha hizo zilitolewa kwenye Mkutano wa Maafisa Elimu hao uliofanyika Manispaa ya Morogoro.

Akikabidhi fedha hizo, Mchengerea amesema, “Maafisa Elimu kwa ushirikiano wao waliona umuhimu wa kuchangishana na kusaidia waathirika wa maafa yaliyotokea Hanang na kunituma nikukabidhi wewe Mhe.Waziri mwenye dhamana.”

Naye Waziri Mhagama amewashukuru kwa mchango huo na kuunga mkono serikali katika kuhudumia wananchi hao na kwamba fedha hizo zimewekwa kwenye Akaunti ya maalum ya maafa iliyoko Benki Kuu.

Polisi wahofia idadi ya vifo wanaojinyonga kila wiki
15 wafariki kwa ajali ya Basi, Daladala