Ofisi ya Rais imesema, Waziri wa mambo ya nje wa Zambia, Stanley Kakubo amejiuzulu baada ya kukumbwa na kashfa kwenye mitandao ya kijamii akidaiwa kufanya makubaliano na Mfanyabiashara wa Kichina, Zao.

Kakubo, mwenye umri wa miaka 43, alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje tangu Septemba 2021, na katika barua yake amesema ameacha kazi kwa sababu ya tuhuma mbaya kuhusiana na shughuli za kibiashara.

Picha za video zilizosambaa haraka kwenye akaunti za mitandao ya kijamii Nchini Zambia zikimuhusisha Waziri huyo, ziliwaonesha watu wawili wakihesabu pesa zilizokuwa zimepangwa mezani ambao ulichapishwa mtandaoni Julai 8, 2022.

Ujumbe huo uliitaja kampuni ya madini ya Kichina na kampuni ya madini ya Zambia na ukisema kuwa wamebadilishana dola 100,000 na hata hivyo majina ya Kakubo na Zang hayakuwemo kwenye chapisho hilo.

Adel Amrouche: Tunajua nini cha kufanya AFCON 2023
Wapewa darasa usafirishaji salama wa Kemikali