Mtaalam wa masuala ya kiteknolojia katika Benki ya Cooperative nchini Kenya, Simon Seno ameshtakiwa kwa tuhuma za kufichua siri na wizi wa akaunti ya mmoja wa wateja, Nancy Kihanya kiasi cha KShs. 2.2 Milioni.

Seno, ambaye pia ni afisa IT katika benki hiyo alishtakiwa pamoja na Harrisson Njoroge na Barack Ochieng ambaye hakufika kortini, walikabiliwa na shtaka la kushiriki uhalifu kwa kutembelea matawi mengi ya Benki ya Cooperative na kuiba wakitumia teknolojia ya kimtandao.

Wawili hao walioshtakiwa mbele ya Hakimu Mwandamizi wa Mahakama hiyo, Gilbert Shikwe walikanusha mashtaka sita na dhamana yao ilizuiliwa, ili kutopindisha ushahidi wa kesi hiyo inayowakabili.

Katika shtaka la kuunda njama za kuibia kiasi hicho cha fedha, Seno na Njoroge walishtakiwa pamoja, lakini Seno alishtakiwa peke yake kwa kuvuruga mitambo ya kompyuta ya benki hiyo ili kufanikisha zoezi.

Hata hivyo, Kongozi wa mashtaka, Judy Koech alisema kesi hiyo itaunganishwa na nyingine inayosikilizwa na Hakimu mwandamizi, Martha Nanzushi.

Ndejembi aagiza uchunguzi fedha za ujenzi
Bodaboda waulizwa kama wapo tayari