Madereva mmejiandaa? Ni swali lililoulizwa na Polisi Kata wa ya Ruhembe Tarafa ya Mikumi Mkoa wa Morogoro, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Flora Shayo kwa Vijana wa Bodaboda wa kijiwe cha Kidogobasi alipotembelea kwa lengo la kutoa elimu.

Elimu iliyotolewa kwa mfululizo mwaka 2023 na Polisi Kata huyo kwa Vijana wa Bodaboda imepelekea ukaribu dhidi yao na kupunguza uhalifu kwa kiwango kikubwa jambo ambalo limepelekea Shayo kuwafikia tena na kuweka mikakati ya kuzuia uhalifu kwa mwaka mpya wa 2024.

Hamisi Mustapha, bodaboda wa kijiwe cha Kidogobasi wakati akijibu swali la Polisi Kata huyo amesema wataendelea walipoishia na safari hii mkazo mkubwa watauweka kwenye kutoa taarifa za wahalifu, kuwaripoti wanao wabebesha mizigo ya wizi na uhalifu mwengine.

Naye David Johnson amesema atakuwa mlinzi wa watoto wakike wanakwenda na kurudi shule kila siku ili wafikie ndoto zao na kwa pamoja waliweka maazimio ya kupunguza matukio ya kihalifu au kuyamaliza kabisa.

Afisa wa Benki Mahakamani kwa kumuibia Mteja
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Januari 14, 2024