Kocha Mkuu wa Simba SC, Abdelhalk Benchikha amechukizwa na kitendo cha timu yake kupoteza katika mchezo wa fainali na kupelekea kushindwa kuubeba ubingwa wa michuano ya Mapinduzi uliokwenda kwa timu ya Mlandege iliyobeba ubingwa huo mara mbili mfululizo.
Kocha Benchikha amesema kuwa hajafurahiswa na kikosi chake kushindwa kupata ubingwa huo huku pia akiweka wazi kuwa wanatakiwa kufanya maboresho makubwa ya kikosi chake ili kuendana na kasi jambo ambalo litalazimu baadhi ya wachezaji kuachwa ili waje wengine.
Katika mchezo huo wa fainali uliopigwa juzi Jumamosi (Januari 13) katika Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar, Simba SC walikubali kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 kutoka kwa Mlandege ambao
“Matokeo hayajakuwa mazuri kwa upande wetu na tumeona ni kwa jinsi gani timu yetu imeshindwa kufanya yale ambayo wengi waliyatarajia, na hii ni kutokana na kutokuwa na kikosi sahihi cha ushindani.
Tulihitaji kuwa mabingwa, tulitakiwa kushinda hii fainali kwa namna yoyote, lakini kwenye malengo yetu tulitakiwa kucheze mchezo mzuri na tushinde ubingwa, lakini utaona yote tulivikosa.
“Wachezaji wamepata muda mwingi wa kuonyesha uwezo wao hadi kwa wale ambao walikuwa hawapati nafasi ya kucheza, nafikiri sasa yanawezwa yakafanywa maamuzi sahihi, tunatakiwa kuifanya hii timu kuwa tishio kwani kwa sasa bado timu haijawa imara,” amesema kocha huyo.