Waziri wa uchukuzi wa Singapore S.Iswaran amefunguliwa mashtaka 27 ya ufisadi, katika mojawapo ya kesi kubwa za ufisadi zinazomkabili kwa miongo kadhaa, huku akiamua kuchukua uamuzi wa kujiuzulu.

Katika barua yake, Iswaran amesema anayapinga mashtaka hayo na kwa asa atajikita katika kulisafisha jina lake, tukio ambalo limewashangaza Wanachi wa Taifa hilo kutokana na Wafanyakazi wa Umma kulipwa mishahara mikubwa, ili kuepuka ufisadi.

Shirika la Kuchunguza Visa vya Ufisadi nchini humo – CPIB, limesema Waziri huyo aliyejiuzulu na ambaye alikamatwa Julai 2023, anadaiwa kupokea rushwa ya zaidi ya dola 280,000.

Aidha, inadaiwa kuwa iwapo Iswaran atahukumiwa, huenda akatozwa faini ya hadi dola laki moja za Singapore au kifungo cha miaka 7 jela na visa vya ufisadi ni nadra kutokea nchini Singapore.

TRRH kuweka kambi huduma za matibabu, uchunguzi
Karim Benzema amshitaki waziri Ufaransa