Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amesema kuwa Mwekezaji yeyote atakayezembea kulipa kodi ya pango katika vitalu vya Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) atatolewa ili apewe mwekezaji mwingine mwenye uwezo wa kuendeleza eneo hilo.
Ulega ametoa kauli hiyo wakati wa hafla ya uzinduzi wa programu ya kopa Ng’ombe lipa maziwa iliyofanyika wilayani Karagwe Mkoani Kagera , 2024 ambapo alikabidhi Ng’ombe hao kwa Kampuni ya Kahama Fresh ambao watakopeshwa vijana na Wanawake waweze kujikwamua kiuchumi kupitia uzalishaji wa maziwa.
“Yeyote atakayezembea katika vitalu hivyo, halipi kodi, hafanyi uwekezaji wowote wa maana, anaacha mapori na vichaka, hatujui ana ng’ombe wangapi, anapeleka soko gani, tutamtoa tumuweke mtanzania mwingine atakayeweza kufanya kazi hiyo,” alisema.
Ng’ombe 300 ni awamu ya kwanza ya ngombe 600 ambao watawakopesha wafugaji, ili waweze kuzalisha maziwa na kupeleka malighali kwenye kiwanda cha Kahama Fresh.