Uongozi wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans umeweka wazi kuwa upo tayari kuwapa burudani mashabiki wa timu hiyo kwenye mechi za ushindani kitaifa na kimataifa.

Chini ya Kocha Mkuu, Miguel Gamondi,  Young Africans baada ya kucheza mechi 11 za ligi ilipata ushindi katika mechi 10 na kupoteza mchezo mmoja.

Ipo wazi kwamba katika timu zilizopo tatu bora, kuanzia Azam FC inayoongoza ligi na Simba SC iliyo nafasi ya tatu kwenye mzunguko wa kwanza zote zilifungwa na Young Africans msimu huu wa 2023/24.

Afisa Habari wa Young Africans, Ali Kamwe amesema kuwa wapo kamili kwa ajili ya kuendelea kupata matokeo kwenye mechi zote watakazocheza.

“Kuendelea kuwapa burudani mashabiki wa Young Africans hilo kwetu ni jambo la msingi na ukichagua kuwa Young Africans maana yake umechagua burudani. Tupo kamili gado kuendelea kufanya kweli kitaifa na kimataifa.

“Wachezaj wapo tayari na furaha yao ni kuona timu inapata matokeo. Muda wa maandalizi upo na ligi itakaporejea nasi tutakuwa imara, mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi kila wakati.”

AFCON 2027 – TFF yaitwa mezani kuyajenga
Sababu vifo vya ghafla, matukio ya ukatili zatajwa