Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi Nchini Kenya, Douglas Kanja amesema Watu watatu wamefariki na wengine 271 kujeruhiwa kufuatia ajali ya moto mkubwa uliosababishwa na mlipuko wa gesi usiku wa kuamkia Februari 2, 2024 jijini Nairobi.

“Takriban watu 271 wamelazwa katika hospitali mbalimbali jijini Nairobi na watu watatu wamefariki, serikali ilisema watu 222 walijeruhiwa na wengine wawili kufariki,” alisema Kanja.

Naye Msemaji wa Serikali ya Kenya, Isaac Maigua aliandika katika ukurasa wake kuwa, Moto huo ulizuka usiku wa manane, ukisababishwa na Lori lililojaa gesi iliyolipuka, na kuenea kwa haraka eneo la Embakasi, lililopo Wilaya ya mji Mkuu wa Kenya.

“Moto uliharibu magari na mali kadhaa za biashara, zikiwemo biashara nyingi ndogo na za kati. Kwa bahati mbaya, nyumba za makazi katika eneo hilo pia ziliteketea, na idadi kubwa ya wakazi walikuwa bado wakiwa ndani kwani ilikuwa usiku,” alisema shuhuda Isaac Mwaura.

Hata hivyo, Rais wa Kenya, William Ruto amewalaumu na kuwakashifu Maafisa wa serikali akisema ni watepetevu na Mafisadi kwani walitoa leseni za kujengwa kwa kituo cha gesi kwenye makazi ya watu, wakati ni kosa kisheria.

Usajili Simba SC wamtisha Kitambi
Bosi wa Chelsea amfungia vioo Pochettino