Kocha wa timu taifa ya Mali, Eric Sekou Chelle, amesema anapaswa kuwajibika baada ya kikosi chake kutolewa katika Michuano Kombe la Mataifa Afrika ‘AFCON 2023’, inayoendelea nchini lvory Coast.

Mali iliondoshwa katika michuano hiyo kufuatia kichapo cha mabao 2-1, dhidi ya wenyeji lvory Coast, katika mechi ya Robo Fainali iliyopigwa mwishoni mwa juma lililopita katika Uwanja wa Bouake, Ivory Coast.

Kocha huyo amesema matokeo ya mchezo huo yamemhuzunisha hivyo anapaswa kuwajibika.

“Sikufurahia matokeo hayo, yalikuwa matokeo mabovu pamoja na kuwa na uhaikika wa kufanya vizuri na kufuzu hatua iliyofuatia,” amesema.

Aliongeza kuwa: “Hakuna aliyefurahia kuondolewa kwa timu yetu, nitawajibika kwa matokeo mabovu kwani lengo lilikuwa kufuzu Nusu Fainali kisha Fainali.”

Amesema anaomba radhi na anakwenda Bamako kuzungumza na viongozi wa Shirikisho la Soka nchini Mali na kujua hatima yake.

Mchengerwa azindua mfumo ufundishaji mubashara
Mahundi: Mradi wa Maji Tukuyu kuhudumia wakazi 63,647