Serikali imesema inaendelea na ukamilishaji wa Mradi wa Maji Tukuyu Mjini, unaolenga kuhudumia wakazi wapatao 63,647 waishio kwenye Mitaa ya Mabonde, Kasyeto, Ndyonga, Batini, Bulyaga, Makandana.

Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Maryprisca Mahundi ameyasema hayo hii leo Februari 7, 2024 Bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la mbunge wa Rungwe, Anton Mwantona aliyeuliza ni lini mradi wa maji Tukuyu utakamilika.

Akijibu swali hilo, Mhandisi Mahundi amesema utekelezaji wa mradi huo umefikia wastani wa asilimia 85 ambapo kazi zilizo tekelezwa hadi sasa ni pamoja na ujenzi wa banio katika chanzo cha Mto Mbaka, uchimbaji wa mtaro na ulazaji wa bomba kuu kutoka kwenye chanzo kwenda kwenye tenki umbali wa Kilometa 9.5.

Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Maryprisca Mahundi.

Aidha ameongeza kuwa, kazi nyingine ilifofanyika ni pamoja na uchimbaji wa mtaro na ulazaji wa mabomba ya usambazaji umbali wa Kilometa 20 pamoja na ununuzi na ufungaji wa dira mpya za maji 125.

“Kazi zilizosalia ni ujenzi wa tenki la kuhifadhia maji lenye uwezo wa lita 1,500,000 pamoja na ununuzi na ufungaji wa dira zingine mpya 5,875 ambapo kazi zote hizi zinatarajiwa kukamilika Mwezi Aprili, 2024” amesema Mahundi.

Eric Sekou Chelle: Nipo tayari kuwajibika
Real Madrid yachizika kwa Mbappe