Mkurugenzi wa Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe Ofisi ya Rais – TAMISEMI Dkt. Rashid Mfaume amesema lengo la Mkutano Mkuu wa Waganga Wakuu Wafawidhi wa Vituo vya kutolea huduma za Afya Msingi Tanzania Bara ni kupata taarifa ya Mifumo ya Uendeshaji wa bidhaa za Afya, Masula ya Ustawi wa Jamii na Lishe, Hali ya Utekelezaji wa afua za Afya, pamoja na Mifumo ya bidhaa za Afya.
Dkt. Mfaume amesema hayo jijini Dodoma wakati akitoa taarifa fupi kwa mgeni rasmi ambaye ni Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu katika Mkutano wa wa Waganga Wakuu Wafawidhi wa Vituo vya kutolea huduma za Afya Msingi.
Mkutano huo, pia ulesezesha kutoa taarifa ya maboresho mbalimbali yanayoendelea katika mifumo ya utoaji wa huduma za afya na pia tumeutumia kama fursa ya kupokea maoni ya wataalamu hao.
Aidha, Dkt. Mfaume pia alisema uwepo mkutano huo muhimu wametoa fursa kwa Wizara zote mbili Ofisi ya Rais – TAMISEMI na Wizara ya Afya pamoja na wadau kutoa mrejesho wa shughuli wanazozifanya za usimamizi, ufuatiliaji wa huduma za afya, Ustawi wa Jamii na Lishe katika maeneo yao.