Mkuu wa Mkoa Kagera, Fatma Mwassa amezindua mradi wa shilingi Milioni 892 unaofadhiliwa TCRS, utakao wezesha kurejesha miundombinu ya makazi, mfumo wa chakula, huduma za maji safi,elimu, afya na usafi wa mazingira pamoja na msaada wa kisaikorojia kwa wathirika wa mvua ya upepo mkali iliyotokea Oktoba 2023 katika Wilaya Bukoba na Muleba.
Akizungumza wakati wa kuzindua mradi huo ulioanza Oktoba 19, 2023 na unaotarajiwa kukamilika Oktoba 19, 2024 Mwassa amesema utakuwa msaada mkubwa wa wakazi walio athiriwakatika kaya 482 ambapo serikali ilifanikiwa kurejesha baadhi ya miundombinu ambayo haikukidhi mahitaji yote.
Aidha katika hatua nyingine RC Mwassa ameishukuru Daiyosisi ya Kaskazini Magharibi pamoja na ELCT inayo ongozwa na Askofu, Dkt. Abedinego Keshomshara kwa kufanikisha kuanzisha mradi huo kwa kuwasaidia wanchi pamoja na TCRS, ili kurejesha hali zao za maisha kwa kuzifanya kuwa bora zaidi.