Johansen Buberwa – Kagera.

Baadhi ya Wananchi wa Mtaa wa Kilimahewa uliopo eneo la Mtakuja, wameiomba Serikali ya Wilaya ya Bukoba Mkoani Kagera kuingilia kati na kuwanusuru na Mbwa wakali wanaozurula mitaani, ambao wageuka kuwa tishio hasa kwa Wanafunzi wanaoenda shuleni nyakati za asubuhi.

Wakizungumza na Dar24 Media, wazazi hao akiwemo Peradius Peningtoni, Bestina pamoja na Philimon Byarugaba wamesema mpaka sasa Watoto saba wameshajeruhiwa na Mbwa hao mtaani kwao, jambo ambalo linaleta hofu ya kuwapelekea watoto wao shule pindi kunapokucha.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Kilimahewa, Edwin Gabrial amesema zoezi la kuwauwa mbwa ambao waliokuwa wanag’ata watu limefanyika kwa kuwapa Nyama yenye sumu, huku akitahadharisha wamiliki wa wanyama hao kuwatunza ipasavyo.

Simba SC kufumua rekodi Abidjan
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Februari 21, 2024