Bilionea, Sir Jim Ratclife amesema kazi yake ya kuirudisha Manchester United kwenve anga za juu na kutamba ndani na nje ya England inaanza sasa.

Tajiri hiyo ameshakamilisha umiliki wake wa klabu ya Man United kwa asilimia 27 baada ya kuweka mzigo wa Pauni 1.3 bilioni kwenye kikosi hicho chenye maskani yake Old Trafford.

Bosi huyo amepitishwa na Ligi Kuu England pamoja na kuthibitishwa na chama cha soka cha England kama tajiri mpya wa Man United baada ya kukidhi vigezo vyote.

Sir Jim alisema: “Kuna mmiliki mwenza wa Manchester United ni heshima kubwa na hili linahitaji kuwajibika kwa kiasi kikubwa. Kukamilika kwa jambo hilo ni mwanzo wa kuanza safari ya kuirudisha Man United kwenye anga za juu za soka la England, Ulaya na dunia. Kazi ya kufikia hayo imeanza rasmi.”

Na Mwenyekiti mtendaji mwenza wa miamba hiyo, Joel Glazer anatarajia makubwa kutokea kwenye kikosi cha Man United baada ya tajiri Ratcliffe kuingia kwenye bodi ya timu hiyo.

Joel Glazer alisema: “Ningependa kumkaribisha Sir Jim kama mmiliki mwenza, tunasubiri kwa hamu kufanya kazi kwa ukaribu kwa ajili ya hatima nzuri ya Manchester United.”

Ratcliffe tayari ameshaanza shughuli za kisoka kwenye klabu hiyo. Kupitia kampuni yake ya INEOS tayari amefanya mchakato wa kumnasa Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Man City, Omar Berrada.

Uhusiano Urusi, Tanzania kuzinufaisha pande mbili - Dkt. Nchimbi
Mastaa Barcelona kupigwa bei