Wanasema hakuna cha bure. Hivyo ndivyo alivyosema tajiri mpya wa Manchester United Sir Jim Ratcliffe ambaye kwa mujibu wa tovuti ya Daily, amempa mtendaji mkuu mpya wa Man United, Omar Berrada maagizo makali.

Ratcliffe amemtaka Berrada kuzingatia sana masuala ya pesa hususan kwenye mishahara ya wachezaji na kusisitiza anatakiwa awape bonasi ikiwa tu watafanya vizuri.

Tangu achukue umiliki na kupewa nguvu ya kusimamia masuala yote ya soka tajiri huyu alieleza anataka kufanya mabadiliko kwenye sehemu nyingi ikiwa pamoja malipo.

Man United ilifanya vibaya kwenye michuano mbalimbali na kombe la Carabao Cup ililobeba msimu uliopita lilikuwa ni taji lao la kwanza baada ya miaka kadhaa kupita.

Berrada ambaye amejiunga na Man United akitokea kwa majirani zao Manchester City anataka kuhakikisha mbinu alizokuwa akizitumia Man City ambazo zilisababisha washinde mataji manne msimu uliopita ndio azitumie kwa Man United kuhakikisha wanafanikiwa.

Katika ripoti yao ya kifedha inaonyesha kuwa Man United ilitumia Pauni 330 milioni kwenye mishahara lakini hakuna mafanikio waliyoyapata.

Man City ambayo ilitumia Pauni 400 milioni katika ripoti yao iliyochapishwa Novemnba mwaka jana walifanikiwa kupata Pauni 300 milioni kama zawadi za kushinda michuano mbali mbali.

Berrada ameshaonyesha kwamba ana uwezo mzuri wa kufanya mazungumzo na kushawishi wachezaji kusaini kwa bajeti ndogo hali ambayo ni tofauti kwa Man United ambayo mara zote imekuwa ikivunja benki kusajili mastaa wapya ambao pia imekuwa ikiwalipa mshahara mkubwa.

Teknolojia: Wafurahia masomo Kidijitali Chalinze
Bukayo Saka awajibu wachambuzi