Scolastica Msewa, Chalinze – Pwani.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete amepokea msaada wa Kompyuta Mpakato 80 zenye thamani ya Shilingi million 71 zilizotolewa na Shirika lisilo la kiserikali la Reneal International Education Outreach la Nchini Marekani kwa ajili ya Shule nne za Sekondari zilizopo Halmashauri ya Chalinze.

Msaada huo, umetolewa wakati akizindua mradi wa matumizi ya Kompyuta hizo katika makabidhiano ya vifaa vya TEHAMA kwa shule hizo nne katika shule ya Sekondari ya Mboga ambayo imekabidhiwa kompyuta mpakato 20.

Amesema, kompyuta hizo zinakwenda kurahisisha upatikanaji wa taarifa za masomo na kuwezesha Walimu na wanafunzi kupata elimu kwa njia ya kisasa na rahisi hasa rejea ya masomo na mitihani yote ya taifa ya kidato cha pili na Nne.

“Lengo kubwa la kuanzisha maabara za kompyuta (TEHAMA) kwenye shule za sekondari hizo ni kusaidia ujifunzaji kwa wanafunzi na kwa walimu ufundishaji wa masomo ya sekondari hususani masomo ya sayansi,” alisema Ridhiwani.

Kwa nyakati tofauti,Mratibu wa shirika hilo na Afisa TEHAMA wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, David Nyangaka wamezitaja shule za Sekondari zitakazonufaika na mradi huo kuwa ni pamoja na Msata, Mdaula na Mandera huku kila kompyuta ikiwa na mitihani ya kitaifa iliyofanyika nchini kuanzia mwaka 1988, ili wanafunzi watumie kujisomea.

Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Februari 27, 2024
Mambo mazuri yanukia Old Trafford