Afarah Suleiman, Babati – Manyara.

Mkuu wa kituo cha Polisi cha Babati Mkoani Manyara, ASP. Amiri Mlemba amewapongeza Wananchi wa Mtaa wa Mruki uliopo Kata ya Maisaka, kwa kuimarisha ulinzi na usalama wa eneo lao ambalo halina matukio ya ukatili.

Mlemba ameyasema hayo katika kikao na Wananchi wa Kata hiyo na kudai kuwa wanapanga kuwajengea kituo cha Polisi, ili kusaidia zaidi kuendelea kuimarisha usalama.

Aidha, amewataka Wananchi kuondoa hofu ya kufika kwenye vituo vya Polisi kuwaweka dhamana ndugu zao pale wanapokamatwa kwa makosa mbalimbali, kwani Askari ni mlinzi wa raia na mali zake.

Kwa upande wao Wanananchi wa Kata hiyo wametoa shukrani kwa namna Jeshi hilo linavyowapq ushirikiano pindi wanapoomba msaada wa kiusalama.

Rais Mstaafu Mzee Mwinyi afariki Dunia
Waziri Mkuu wa Ethiopia awasili Nchini kwa ziara ya Kitaifa