Rais Mstaafu wa awamu ya pili Tanzania, Alhaj Ali Hassan Mwinyi amefariki dunia hii leo Februari 29, 2024.

Taarifa za kifo cha Mzee Mwinyi zimetanganzwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati akilihutubia Taifa kupitia Vyombo mbalimbali vya Habari.

Amesema, kifo hicho kimetokea katika Hospitali ya Mzena Jijini Dar es salaam alikolazwa kwa matibabu ya Saratani ya Mapafu Februari 29, 2024.

 

Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Machi 1, 2024
Polisi wakubali kazi ya Wananchi Maisaka