Wagombea 14 waliochukua fomu za utezi kuwania udiwani Kata ya Kimbiji katika Halmashauri ya Wilaya ya Kigamboni Mkoani Dares Salaam wamerejesha fomu na kuteuliwa kuwania nafasi hiyo, katika uchaguzi Mdogo wa udiwani utakaofanyika Machi 20, 2024.
Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi Kata ya Kimbiji, Ricky Pascal amesema wagombea hao walianza kuchukua fomu za uteuzi kama Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilivyopanga Februari 27,2024 hadi leo Machi 4,2024 na wote kukamilisha ujazaji fomu na kuzirejesha.
Walioteuliwa ni Rachel Paulo Mwikola (UPDP), Halima Abdallah Mbago (NLD), Shabani Hassan Chumu (Demokrasia Makini), Kondo Abdu Hatibu ‘Lukali’ (CUF), Diana-Rose Joseph Mhoja (ADA Tadea), Maimuna Mwinyipingu Yusufu (CCM) na Shani Ally Kitumbua (AAFP),
Wengine ni Michael Makile Mzalendo (UDP), Joyce Ephraimu Mweigule (DP), Janeth Pius Mhando (TLP), Nasra Twalib Kimo, Innocent Fratern Shirima (CCK), Neema Kassimu Yegeyege (UMD) na Juma Hassan Abdalah (NCCR-Mageuzi).
Tume ilitangaza uchaguzi Mdogo katika Kata 23 za Tanzania bara kufanyika Machi 20,2024 na fomu za uteuzi zilianza kutolewa Februari 27 hadi Machi 4 mwaka huu na Wagombea hao, walikabidhiwa fomu zao za uteuzi na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi Kata ya Kimbiji, Ricky Pascal na Twidike Ntwima.