Arsenal inataka kumsajili Kiungo Mshambuliaji kutoka Brazil na Klabu ya Barcelona Raphael Dias Belloli ‘Raphinha’, na Mshambuliaji wa timu hiyo, Ferran Torres katika dirisha lijalo la majira kiangazi kwa ajili ya kuboresha la ushambuliaji.

Mara kadhaa Barca imekuwa ikihusishwa kuwa na mpango wa kuuza baadhi ya mastaa kutokana na hali mbaya ya kiuchumi inayowaandama.

Licha ya kuhusishwa kuondoka, mastaa hao wameonyesha viwango bora kwenye kikosi cha kwanza cha Barca tangu kuanza kwa msimu huu.

Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta amekuwa akihitaji kuboresha eneo la ushambuliaji tangu dirisha la majira ya kiangazi msimu uliopita kwa sababu mastaa alionao wamekuwa wakikumbwa na majeraha mara kwa mara.

Mkataba wa sasa wa Raphinha mwenye umri wa miaka 27, unatarajiwa kumalizika 2027.

Msimu huu amecheza mechi 25 za michuano yote na kufunga mabao matano huku Torres msimu huu amefunga mabao 11 katika mechi 32.

Uanachama wa Somalia EAC: Makamba ampa neno Waziri Jama
Makonda azishukia Wizara, amtaja Mzee Mwinyi