Katibu wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo CCM Taifa, Paul Makonda amekutana na kuzungumza na Wanahabari hii leo  Jumanne Machi 5, 2024 ambapo amezungumzia mambo mbalimbali ikiwemo yale aliyoyaona katika ziara yake ya kuzunguka mikoani kusikiliza na kutatua kero za Wananchi na zifuatazo ni baadgi ya nukuu muhimu alizozitoa.

1.”Iko dhuluma kubwa kwenye sekta ya ardhi nchini, huko kumekithiri kwa kuwa kilio cha watu kunyang’anywa maeneo yao, kilio cha watu kupewa nyaraka au hati feki, hilo tumetoa maelekezo mahsusi, tulimwelekeza Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Jerry Silaa aende na aweke utamaduni wa kuhangaika, na hilo tulifanya hata tulipoanza ziara yetu ya kwanza kabisa pale Dodoma tulimwelekeza naye alifanya usiku na mchana asisite achukue hatua hata kama zina maumivu.” Katibu wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo CCM Taifa, Paul Makonda.

2. “Yapo mambo matatu tumeyabaini kwenye ziara na kwa sasa tunaendelea na ukamilishaji wa ripoti, ili tuweze kumkabidhi Dkt. Emmanuel Nchimbi, kwa Mwenyekiti wetu wa chama na Wajumbe wote wa Kamati Kuu, wapate kuona hali ya kisiasa na utendaji kazi wa Serikali katika kuwahudumia Wananchi kwenye maeneo yote tuliyotembelea kwenye mikoa 23.” Katibu wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo CCM Taifa, Paul Makonda.

3. “Nianze kwa kukumbuka nukuu ya Dkt. Samia Suluhu Hassan (Mwenyekiti wa CCM Taifa ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania) alipokuwa kwenye msiba wa Mzee Ali Hassan Mwinyi wakati anatoa salamu zake za pole kwa Taifa, kwa familia na chama chetu (CCM), moja ya neno alilolisema kwenye hotuba yake ni kurejea kumbukumbu ya barua ya Mzee wetu Hayati Ali Hassan Mwinyi wakati anamuandikia Rais kuomba kujiuzulu.”

4. “Dkt. Samia aliamua kunukuu hayo maneno, mojawapo ya nukuu aliyoitumia ni kwamba Hayati Mzee Mwinyi alionekana kukubali ya kwamba japokuwa sikuwepo kwenye eneo lakini jambo hili lometokea kwenye Wizara yangu na mimi nilipaswa kulijuwa na kulifahamu kwa haraka, Dkt. Samia akaenda mbele zaidi akasema je watendaji mlioko huko kwenye Wizara mnazijuwa Wizara zenu?, mnawajibika kikamilifu?, maana ni swali la mtego kwamba kila mtu atafakari tunapomuenzi na kumkumbuka Mzee Ali Hassan Mwinyi kwa kazi alizozifanya na heshima na uungwana aliokuwanao je, sisi kwenye nafasi zetu na ofisi zetu tunafanya nini?”

Arsenal kumsajili Raphinha
DAWASA yatangaza upungufu wa Maji Dar es Salaam