Heldina Mwingira.

Mradi wa ujenzi wa reli ya SGR kwa safari za Dar es salaam kwenda Morogoro wenye km 300 umekamilika kwa asilimia 96.35 na yalifanyika majaribio ya safari za treni ya umeme Februari 26, 2024.

Mradi huo wa kihistoria wenye malengo ya kupunguza muda wa kusafiri, ufikiaji rahisi kwa huduma mbalimbali za jamii kwa jumuiya ya eneo la mradi na uwezeshaji wa biashara kati ya Tanzania na nchi za jirani ulianza mwaka 2017 katika awamu ya tano iliyokuwa ikiongozwa na  hayati  Dkt. John Pombe Magufuli.

Hatua  ya ujenzi wa mradi huo umeendel;ezwa chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu aliyeingia na kauli mbiu yake ‘kazi iendelee’ kwa kuendeleza miradi yote aliyoifanya mtangulizi wake ambaye alifariki Machi 17, 2021.

Kwa kupitia mradi huu wa reli wa kietroniki ya kisasa watu mbalimbali wenye ujuzi wamepata ajira za kudumu na za  kimkataba na Wahudumu wa ndani ya treni hio ni sehemu ya watu walionufaika na ujio wa mradi huo na  katika majaribio yake.

Mitandao ya kijamii ya Shirika la reli Tanzania  ilituonesha wahudumu wanawake wakiwa wmepiga picha ya pamoja vilevile vyombo vya habari mbalimbali na watu binafsi viliendelea kuchapisha picha na video za wahudumu hao.

Hata hivyo, kuonekana kwa picha  na video hizo, kukazua gumzo katika  mitandao ya kijamii na kusababisha wahudumu hao kupata kadhia ya kufanyiwa ukatili wa mtandaoni,  kwa kutukanwa, kutolewa maneno yasiyo na staha, matamshi ya chuki yenye unyanyasaji wa kimtandao.

Baadhi ya Watu walitoa maoni yao kwa kutumia lugha isiyo na staha inayomaanisha shirika la Reli la Tanzania litafute wahudumu wengine wa kike  kwa sababu mionekano ya wahudumu wa sasa ya mwili na sura haiwavutii huku wengine wakiisisitiza serikali ikiwa inachagua wahudumu izingatie urembo wa sura na maumbo mazuri ya mwili.

Ukatili kama huu, ulishawahi kutokea mwaka 2020 kwa wahudumu wa Ndege katika mtandao ya kijamii na kujadiliwa Bungeni hali iliyopelekea  Ladislaus Matindi ambaye ni  Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege Nchini (ATCL), kujitokeza na kufafanua.

Alisema, Muhudumu wa ndege anahitajika awe uwezo wa kuzingatia usalama wa abiria na  wa ndege,  awe mwepesi  na  awe anajua kuogelea, awe  na urefu usio chini wa futi 5.2 vilevile alinukuliwa akisema “uzuri wa mtu ni uwezo wa kufanya kazi.”

Kutokana na matukio haya yanayoendelea katika jamii yetu inaonesha kuwa ukatili dhidi ya wanawake mtandaoni ni kitu cha kawaida na kisichokuliwa uzito  na jamii.

Ikumbukwe kuwa, kumfanyia mwanamke ukatili mtandaoni ni kosa kisheria kama inavyoainishwa katika  Sheria ya Maudhui ya Mitandaoni (Online Content Regulation) 2020  na Sheria ya Kimakosa ya Mtandao 2015 (Cyber Crime Act).

Watu wanatakiwa kuwa makini na vitu vya kuandika mtandaoni, ili wasije wakaingia katika mkono wa sheria na kuhusu hili la Mradi wa reli ya kisasa, Mradi bado unaendelea na utapita maeneo mbalimbali kama vile Makutopora (Dodoma), Tabora, Isaka (Shinyanga), Mwanza, Rusumo (Kigali,Rwanda), Bujumbura.

Hivyo  wahudumu wa kike wa wataendelea kuajiriwa,  Jamii inabidi itambue kuwa  katika kuwaajiri wahudumu wa taasisi  huwa wanazingatia uwezo wa mtu kufanya kazi na sio sura na uzodoaji huo usilete madhara kwa wengi kuhofia kusakamwa mitandaoni hivyo kuzima ndoto zao.

Ajali: Ndege zagongana, wawili wafariki
Simulizi: Njia waliyotumia wazazi wangu ili nifaulu masomo