Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini Kenya, imethibitisha madai ya kugongana kwa ndege ya abiria ya Kampuni ya Safarilink na ndege ya mazoezi na tayari uchunguzi umeanza kubaini chanzo cha ajali hiyo.

Idara ya Uchunguzi wa ajali za Anga na Huduma ya Taifa ya Polisi nchini humo, imesema, ‘’Uchunguzi umeanza kupitia mashirika mbalimbali ukiongozwa na  kubaini chanzo cha ajali.’’

Watu wawili waliokuwa kwenye ndege ya mazoezi wote wamefariki dunia, huku abiria 39 na wafanyakazi 5 katika ndege ya Safarilink wakiokolewa hadi eneo salama.

Shirika la ndege la Safarilink kupitia mtandao waX limeandika kuwa muda mfupi baada ya kupaa mwendo wa saa tatu na dakika 45 asubuhi kwa saa za eneo hilo, kishindo kikubwa kilisikika.

Zuchu marufuku Zanzibar
Makala: Uzuri wa mtu ni uwezo wa kufanya kazi, sio sura