Mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira Tanzania Dar es salaam -DAWASA, imetangaza uwepo wa upungufu wa huduma ya maji kwa baadhi ya maeneo yanayohudumiwa na mtambo wa kuzalisha maji wa Ruvu chini ili kuruhusu maboresho ya msingi katika mtambo.

Maeneo ambayo yataathirika na upungufu huo wa huduma ya maji siku tatu mfululizo ni Bagamoyo, Mapinga, Mabwepande, Bunju, Tegeta, Kunduchi, Mbweni, Boko, Salasala, Goba, Mivumoni, Madale Kawe, Lugalo, Makongo, Chuo kikuu UDSM, Mwenge na Chuo kikuu Ardhi.

Maeneo mengine ni pamoja na Kijitonyama, Mikocheni, Msasani, Osterbey, Masaaki, Mwananyamala, Kinondoni, Magomeni, Kigogo, Chang’ombe, Keko, Kurasini, Kigamboni, Airport, Kiwalani, Vingunguti, Buguruni, Ilala na katikati ya mji.

Makonda azishukia Wizara, amtaja Mzee Mwinyi
Watalii wa kigeni wavunja rekodi Hifadhi ya Urithi wa Dunia