Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans leo Jumatatu (Machi 11) wanashuka Uwanja wa Azam Complex, Dar es salaam kuikabilia Ihefu FC katika mchezo wa Ligi Kuu kuanzia saa 12:00 jioni.
Young Africans wanaingia kwenye mchezo huo wakiwa kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo wakikusanya pointi 46 huku wageni wao Ihefu wakiwa nafasi ya nane na pointi zao 23.
Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza uliofanyika Uwanja wa Haighland Estate Mbarali, Young Africans ilifungwa mabao 2-1 na lhefu, hivyo leo itaingia kwa lengo la kuchukua pointi tatu na kulipiza kisasi cha kupoteza mchezo huo.
Kuelekea mchezo huo Kocha Mkuu wa miamba hiyo ya soka nchini Miguel Gamondi amesema maandalizi yao yamekamilika na lengo lao ni moja tu ambalo ni kupata ushindi utakao wafanya kuendelea kukaa kileleni na kuwapa furaha mashabiki wao.
Tunajua lhefu ndiyo timu pekee iliyotujeruhi msimu huu, lakini tumejipanga kulipa kisasi na kutanua uongozi wa ligi, binafsi sikufurahi tulivyopoteza nchezo wetu dhidi yao kule kwao, safari hii tunataka machungu yawe upande wao.” amese ma Gamondi
Kwa upande wake Kocha Mkuu wa lhefu Mecky Maxime amesema utakuwa mchezo mgumu kutokana na ubora waliokuwa nao Young Africans hivi sasa.