Mshambuliaji kutoka nchini Misri na Klabu ya Liverpool Mohamed Salah amesema ataondoka kwenye klabu hiyo ya Anfield, lakini sio kwa sababu ya Kocha Jurgen Klopp.

Kumekuwa na tetesi zinazomhusu Salah kuondoka kwenye timu hiyo mwisho wa msimu na atakuwa amebakiza mwaka mmoja mkataba wake kumalizika, na imekuwa ikielezwa mastaa wengi wataondoka kwa sababu Klopp amnetangaza ataachana na timu hiyo.

Hata hivyo, Salah alipoulizwa juu ya kuondoka mwisho wa msimu na klabu kadhaa za Saudi Arabia zinamtaka, alisema hapana.

“Kuondoka ni sehemu ya maisha ya soka. Wachezaji wazuri walishawahi kuondoka kwenye timu hii, tena walikuwa na umuhimu mkubwa kwenye timu, kocha naye pia ana umuhimu wake, pia ataondoka, mimi pia siku moja nitaondoka lakini sio kwa sababu Klopp ameondoka”

Katika dirisha la majira ya kiangazi mwaka jana Salah aliripotiwa kuhitajika na Al-Ittihad ambao waliweka mezani zaidi ya Pauni 150 milioni ili kumnunua, lakini ilikataliwa.

Tangu ajiunge na Liverpool mwaka 2017, Salah amekuwa mmoja wa wachezaji tegemeo kwenye kikosi cha kwanza na hadi sasa amefunga mabao 205 katika mechi 334 alizochezea timu hiyo kwenye michuano mbalimbali.

Pia katika kipindi chote hadi sasa ameshinda taji moja la Ligi Kuu England na Ligi ya Mabingwa Ulaya, Kombe la FA moja na Carabao mawili.

Msimu huu pia huenda akachukuwa kombe lingine kati ya FA Cup, Ligi Kuu England ama Europa League baada ya kubeba Carabao.

Azam FC yaanza kuiwinda Young Africans
Kocha Dabo amkataa mazima Prince Dube