Kiongozi wa Taifa la Caribbean, Kiongozi wa jumuiya ya kikanda na Rais wa Guyana, ametangaza kujiuzulu kwa Waziri Mkuu wa Haiti, Ariel Henry (74), ambaye amekuwa akishililia nafasi hiyo isiyo ya kuchaguliwa, tangu mauaji ya mwaka 2021 ya Rais wa mwisho wa nchi hiyo, Jovenel Moise.

Kujiuzulu kwa Henry, kunajiri baada ya Viongozi wa eneo hilo kukutana katika nchi jirani la Jamaica kujadili mfumo wa mpito wa kisiasa, ambao Marekani ilitaka uharakishwe, huku magenge yenye silaha yakitaka kupindua serikali yake.

Henry, ambaye raia wengi wa Haiti wanamchukulia kuwa fisadi, alikuwa ameahirisha uchaguzi mara kwa mara akisema lazima usalama urejeshwe kwanza ambapo muhula wa mwisho wa Maseneta wa Haiti ulimalizika mwanzoni mwa mwaka 2023.

Haiti ilitangaza hali ya hatari mwezi huu (Machi), huku mapigano yakiharibu mawasiliano na kupelekea wafungwa kutoroka mara mbili Gerezani baada ya Kiongozi wa muungano wa makundi yenye silaha, Jimmy “Barbeque” Cherizier kusema wangeungana na kumpindua Henry.

Polisi, ZUIA wafufua matumaini ya Mwanafunzi Kolahill
OSHA wakamilisha tathmini vihatarishi vya usalama, afya JNHPP