Lydia Mollel – Morogoro.

Mwanafunzi Abdul Abeid wa  kidato cha pili katika shule ya Sekondari Kolahill anayeishi mtaa wa Area 5, Kata ya Kichangani Manispaa ya Morogoro, amefanikiwa kupata mahitaji ya shule aliyoyakosa kwa kipindi kirefu kutokana na hali duni ya maisha katika familia yake, iliyosababisha kusitisha masomo yake.

Mahitaji hayo, yamefanikishwa na Polisi Kata wa Kata hiyo Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Rose Manzi ambaye alichukua hatua za kutafuta msaada kwenye Taasisi zinazosaidia watoto wenye mazingira magumu na kukutana na shirika la “ZUIA HUMAN TRAFFICKING” ambao walikubali kutoa msaada huo, baada ya kujiridhisha uwepo wa hali duni ya maisha katika familia hiyo.

Mwanafunzi Abdul alikuwa na changamoto ya sare na vifaa vingine vya shule pamoja na nauli/usafiri  wa kumfikisha shuleni, ambapo Taasisi hiyo imempatia vitu vyote hivyo huku mchakato wa manunuzi ya Baiskeli na ukataji wa Bima ya Afya ukiendelea.

Familia ya Bi Sikudhani Abeid ina watoto wa 5 wakiishi bila baba na mtoto mwengine mwenye changamoto amemaliza kidato cha nne na kufauli lakini ameshindwa kuendelea kutokana na hali yao, ambapo lakini Taasisi ya ZUIA kupitia muwakilishi wake, Everyin Mwaisakila wameahidi kumsaidi kumpeleka katika Chuo cha VETA.

Simulizi: Nilifukuzwa Chuo kisa kufeli, nimeajiriwa Serikalini
Vurugu zamuondoa Waziri Mkuu madarakani