Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH), Dkt. Alphonce Chandika amewashauri Wananchi kuzingatia mtindo bora wa maisha, ili kulinda figo zao.

Dkt. Alphonce Chandika ametoa wito huo jijini Dodoma, ambapo amesema wananchi wanapaswa wafanye mazoezi kuzingatia mlo usioathiri moyo ili kuzilinda figo.

Amesema, “mtindo bora wa maisha unaozingatia milo isiyoathiri moyo, mazoezi ya kutosha utaisaidia sana kulinda figo zetu”,amesema.

Dkt Chandika amesema kwa siku wamekuwa wakisafisha damu wagonjwa 50 wa figo katika Kitengo cha Kusafisha Damu, Idara ya Magonjwa ya Figo katika hospitali hiyo.

“Watu wenye tatizo la figo wanapaswa kusafisha damu mara tatu (3) kwa wiki kwaajili ya kuendelea kuboresha afya zao”. Amesema Chandika

Dkt Chandika amesema mpaka sasa, BMH imeshafanya oparesheni za upandikizaji figo kwa watu 36 toka huduma hii ianze miaka sita (6) iliyopita.

Mwaka 2019, BMH ilikuwa Hospitali ya pili nchini kuanzisha huduma ya upandikizaji figo, lakini ndiyo Hospitali pekee kutoa huduma hiyo bila usaidizi wa Hospitali za nje.

Siku ya Figo Duniani mwaka huu inaadhimishwa ikiwa na kauli mbiu isemayo “Afya ya Figo kwa Wote pamoja na Upatikanaji Bora wa Matibabu”

Sababu ya samatta kuachwa Taifa Stars
Kamati ya Bunge yaridhishwa ujenzi Mradi wa Umeme Arusha