Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, imeishauri Serikali kuagiza magari yenye mfumo wa gesi ambao una gharama nafuu, hali itakayosaidia kupunguza gharama za mafuta kutokana na uwepo wa Gesi Nchini.
Ushauri huo, umetolewa hii leo Machi 15, 2024 na Mwenyekiti wa kamati hiyo, David Mathayo wakati wa ziara ya kutembelea vituo viwili vya kuzalisha gesi vya Master gas na Taqa Dalbit vilivyopo jijini Dar es salaam.
Amesema, “Tunaishauri Serikali iangalie uwezekano wa magari yake kutumia mfumo wa Gesi, hii itapunguza gharama za mafuta inazotumia na rasilimali ya gesi tunayo ni yetu.”
Naye Naibu waziri wa Nishati, Judithi Kapinga amesema amepokea ushauri na maelekezo kutoka kwenye kamati hiyo ya Bunge na kwamba tayari wamejipanga kuongeza vituo 15 vya kujazia gesi vitakavyokamilika ndani ya mwaka huu.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la Petroli Tanzania – TPDC, Mussa Makame amesema mpango wa kununua vituo vya gesi vitano vyenye uwezo wa kuhama unaandaliwa kuanzia na vitatawanywa maeneo mbalimbali.