Viongozi wa Azam FC leo Ijumaa (Machi 15) wamekutana na kuzungumza na wachezaji wa timu hiyo, ili kuongeza chachu ya kupambana dhidi ya mabingwa watetezi wa Tanzania Bara Young Africans.

Azam FC itakuwa mwenyeji wa mchezo huo keshokutwa Jumapili (Machi 17), Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam, huku ikihitaji kulipa kisasi cha kupoteza mchezo wa mzunguuko wa kwanza kwa kufungwa 3-2 na Young Africans.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari vya Azam FC, Viongozi wa klabu hiyo wamefanya mazungumzo hayo na wachezaji leo mchana katika uwanja wa Azam Complex Chamazi jijini Dar es salaam.

Azam FC ipo nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa na alama 44 ikitanguliwa na Young Africans yenye alama 52, huku Simba SC ikiwa nafasi ya tatu kwa kumiliki alama 42.

Serikali yashauriwa kuagiza Magari yanayotumia Gesi
Arsenal kuivaa Bayern Munich Robo Fainali