Ukraine imeonesha kutofurahishwa na ushindi wa Rais wa Urusi, Vladimir Putin kufuatia Rais wake Volodymyr Zelensky kudai kuwa uchaguzi huo haukuwa halali, akisema Putin amelewa madaraka na atafanya kila mbinu ya kuendelea kuongoza milele.
Kauli ya Zelensky inakuwa wakati ambapo marafiki na washirika wa Putin wakiendelea kumpongeza baada ya kuchaguliwa kwa kishindokuliongoza Taifa hilo.
China ndiyo ilikuwa ya kwanza kumpongeza Putin kupitia Msemaji wa Wizara ya mambo ya kigeni ya Beijing Lin Jian, ikisema nchi hizo mbili ni majirani na washirika wa kimkakati katika kipindi hiki kipya na kwamba marais wa mataifa hayo mawili Xi Jinping na Vladimir Putin, wataendelea kushirikiana katika nyanja mbalimbali.
Naye Rais wa Bosnia, Milorad Dodik amesema watu wake wameukaribisha kwa furaha ushindi wa Putin, kwani ni mtu wa busara na rafiki wanayeweza kumtegemea, huku rais wa Venezuela, Nicholas Maduro akimuelezea Putin kama ndugu yake aliyeshinda kwa kishindo.