Vyama vya upinzani Barani Afrika, vinaweza kuendelea kuzaliwa na kuwepo kwa muda mrefu katika siasa, lakini itavichukua muda mrefu kufanikisha kile ambacho wanahitaji kutokana na baadhi ya Wanasiasa wake kuingia katika migogoro ya ndani na kuishia kufarakana.

Bado haifahamiki kama wanarubuniwa na Vyama Tawala kutengeneza mizozo ya ndani, ama wanapishana kauli kutokana na mambo ya kisera na uwajibikaji wao.

Ushahidi upo, mfano chini Zimbabwe, Nelson Chamisa ameachana na chama chake akitoa sababu mbalimbali ambazo zinaacha maswali, huku Nchini Burundi, Agathon Rwassa akifukuzwa kwenye chama chake.

Huko Uganda, mzozo unaendelea kufukuta ndani ya Chama cha Mwanasiasa maarufu Bob Wine na kilichokuwa chama cha Kizza Besigye cha FDC nacho kimegawanyika na hapa Tanzania mambo si haba kila uchao afadhali ya jana.

Swali kuu ni je, nani yupo nyuma ya migogoro hii, na ni ipi sababu hasa ya kuleta migongano inayosababisha mifarakano isiyo na tija kwa Vyama vinavyopambania maslahi yake na maendeleo ya Taifa?

Ukraine yafadhaishwa na ushindi wa Putin
TAWA yajivunia mafanikio miaka mitatu ya Rais Samia