Mamlaka ya Uhifadhi na Usimamizi wa Wanyamapori Nchini – TAWA, imefanikiwa kukusanya jumla ya TZS Bil. 184.74 katika kipindi cha kati ya mwaka 2020/21 hadi 2024.

Hayo yamesemwa na Kamisha wa Uhifadhi na Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania – TAWA, Mabula Nyanda wakati akitoa wasilisho la mafanikio ya TAWA kwa kipindi cha miaka mitatu (2021/22-2023/24 ) jijini Dar es Salaam.

Amesema, juhudi za kutangaza utalii kupitia filamu ya Royal Tour, Fedha za UVIKO 19 chini ya Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO 19, zimeifaidisha TAWA kwa kuimarisha miundombinu wezeshi ya Utalii.

Miundombinu hiyo ni ile ya maeneo mbalimbali ikiwemo ujenzi wa Kilomita 431.4 za Barabara katika Mapori ya Wamimbiki, Mpanga na Kipengere.

Makala: Vyama kufarakana kuna mkono wa mtu
Imebainika: Komando alifanikisha kifo cha Rais