Klabu ya Azam FC, imeweka wazi dau wanalolitaka kwa timu inayohitaji huduma ya kiungo mshambuliaji wao, Feisal Salum ‘Fei Toto’ kuwa ni dola za Kimarekani milioni mbili sawa na Sh. bilioni 5.l za Tanzania.

Ofisa Habari wa Azam FC, Hashim Ibwe, amesema hawajatangaza kumuuza Fei Toto, lakini kama kuna klabu inamhitaji, italazimika kuvunja mkataba wake kwa kipindi kilichobakiwa, ambao una thamani ya dola za Kimarekani milioni mbili.

Amesema wamekuwa na utamaduni mzuri wa kuwauza wachezaji wao endapo kuna timu inahitaji mchezaji ndani ya klabu yao na wameshafanya hivyo mara kadhaa hapo nyuma.

“Hatujawahi kuwa wachoyo, na mtu ambaye ana mhitaji mchezaji hapa Azam FC, kwa sababu tumekuwa na wachezaji na kuwaacha na kwenda katika klabu mbalimbali wakiwamo Aishi (Manula), Kapombe (Shomari), Erasto (Nyoni), Mudathir (Yahya) na Salum Aboubakar.

“Hatujatangaza ofa juu ya Fei Toto bali kama kuna klabu ambayo inamhitaji kiungo huyo tunawakaribisha waje mezani, tumepiga hesabu na kuona thamani ya mkataba wa mchezaji huyo ni kuona sawa na kiasi hicho,” amesema Ibwe.

Kuna taarifa kuwa Fei Toto ameanza kutajwa katika klabu mbalimbali ikiwamo moja kubwa hapa nchini.

Muundo wa NEMC kuwa Mamlaka washika kasi
Serikali kurejesha Maduka ya kubadilishia fedha za kigeni