Mbunge wa jimbo la Chumbuni Zanzibar, Usi Salum Pondeza hii leo April 2, 2024 Bungeni jijini Dodoma ameibana Serikali ieleleze chanzo kilichosababisha maduka ya kubadilisha fedha kuondolewa katika biashara na wananchi wengi kupoteza ajira zao.

Pondeza pia ametaka kufahamu endapo Serikali ipo tayari kuwarudishia maduka wale waliofungiwa licha ya kuwa hawana shutuma hizo za utakatishaji wa fedha ambao fedha zao na Mali zao zilichukuliwa na Serikali.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Fedha Hamad Hassan Chande ameeleza kuwa baada ya operesheni hiyo, Benki Kuu ya Tanzania ilibatilisha leseni za maduka ya kubadilisha fedha za kigeni yaliyokutwa na makosa.

Amesema mpaka sasa ni maduka saba pekee ndio bado hayajafunguliwa.

Bilioni tano kumng'oa Fei Toto Azam FC
MALIMWENGU: Masikini anapokula jeuri jeuri yake