Johansen Buberwa – Kagera.

Baadhi ya wananchi Mkoani Kagera wameishukuru Serikali kwa kujengwa miradi ya Maji katika maeneo mbalimbali ambayo imewafikia kupitia RUWASA, katika Wilaya za Missenyi na Bukoba.

Wakizungumza na Dar24 Media baadhi ya wananchi hao wamesama kwa sasa hali ya upatikanaji wa maji ni nzuri tofaiti na awali ambapo walikuwa wanatumia maji ya vidimbwi ambayo yaliwasababishia Magonjwa mbalimbali.

Meneja wa RUWASA Wilaya Bukoba, Mhandisi Erasto Mgaya amesema kwa sasa kwenye hali ya upatikanaji wa huduma ya maji imefikia asilimia 78 na miradi saba inaendelea kutekelezwa.

Naye Mhansisi Andrew Kilembe ambaye ni Meneja Ruwasa Wilaya Missenyi amesema utekekezaji wa huduma hiyo ni wa asilimia 78 na miradi 4 inatekelezwa na mpago wa serikali ya awamu ya sita wa kuwafikishia huduma ya maji wanchi mwaka 2025 ni asilimia 85.

Nidhamu, furaha kikwazo Tabora United
Kocha Mashujaa auwekea mipango ukuta wake