Beki wa Manchester United, Raphael Varane, amesema kuumia mara kwa mara katika maisha yake ya soka, kumeharibu mwili wake.

Varane mwenye umri wa miaka 30, aliliamnbia Jarida la Ufaransa Lequipe kwamba amecheza michezo mingi kwa klabu na nchi huku akikabiliana na madhara ya majeraha ya kichwa.

Mchezaji huyo wa zamani wa Kimataifa wa Ufaransa, ambaye alistaafu soka ya kimataifa Februari 2023, alisema alichanganyikiwa wakati akiichezea nchi yake kwenye hatua ya 16-bora ya Kombe la Dunia 2014 dhidi ya Nigeria, na kuongeza kwamba alimaliza mchezo akiwa hajielewi na kwamba “ikiwa kuna mtu alizungumza nami wakati huo, sijui kama ningeweza kujibu.”

Varane alisema pia alicheza akiwa na dalili za jeraha la kichwa akiwa na Real Madrid dhidi ya Manchester City kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu wa 2019-20 ulioathiriwa na COVID-19.

Suala hilo linaendelea kumuathiri Varane na kumfanya akose mechi msimu huu kwa Man United haswa kuhusiana na “mishtuko midogo” inayosababishwa na mipira ya kichwa.

“Mara ya kwanza niliposikia kuhusu kuchanganyikiwa ilikuwa msimu huu ambapo wataalamu walikuja kuzungumza nasi kuhusu hilo mara nyingi, kama mchezaji, hatuelewi na hata hatufikirii kufanya mtihani,” alisema

“Mapema msimu huu, nilipiga mpira kwa kichwa mara kwa mara wakati wa mechi ya Man United na nilihisi uchovu usio wa kawaida katika siku zilizofuata, na pia kuwa na uchovu wa macho.

“Niliripoti kwa wafanyakazi ambao walipendekeza sana nisicheze, na nilifanya mtihani ambao ulimaanisha kwamba nitakosa mechi iliyofuata.”

Mrithi wa Makonda huyu hapa, Hapi arejea kundini
Naymar apanga kurudi nyumbani