Kocha Mkuu wa Singida Fountain Gate, Jamhuri Kihwelu Julio amesema wataingia kwa tahadhari kubwa watakaposhuka Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, kuwakabili Tabora United katika mchezo wa hatua ya l6 bora ya Kombe la Shirikisho Tanzania Bara leo Alhamis (Aprili 04).

Hii itakuwa mechi ya pili kwa Julio kusimama akiwa Kocha Mkuu wa Singida ambayo aliiongoza kushinda mabao 2-1 dhidi va Namungo FC, Uwanja wa Liti kwenye mchezo uliopita wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara.

Julio amesema utakuwa mchezo mgumu na hawataidharau Tabora United kwani ni timu ambayo itakuwa inahitaji matokeo ili kusonga hatua ya Robo Fainali kama wao, hivyo wataingia kwenye mchezo huo wakiwa na tahadhari zote.

“Hivi sasa tunaangalia zaidi mechi hii ili tuweze kushinda na kusonga mbele lengo letu ni kushinda mataji na hili litafanikiwa iwapo kama tutashinda kila mchezo ulio mbele yetu,” amesema Julio.

“Tunajua tunaenda kukutana na timu yenye malengo sawa na sisi, vijana wangu wanajua nini wanapaswa kufanya naamini hawatatuangusha, lengo letu ni kushinda na kwenda Robo Fainali,” ameongeza.

Naye Kocha Msaidizi wa Tabora United, Masoud DJuma amesema kikosi chake kiko tayari kusaka nafasi ya kutinga Robo Fainali na wanaiheshimu Singida Fountain Gate kwani ni timu nzuri, lakini wanaingia kwenye mchezo huo kwa nia ya kushinda ili kusonga mbele.

Marc Brys kocha mpya The Indomitable Lion
Ujenzi SGR umetumia Trilioni 10.69 - Serikali