Mahakama inayoshughulikia kesi za uchaguzi nchini Afrika Kusini, imesema aliyewahi kuwa rais wa zamani, Jacob Zuma anaweza kuwania urais wakati wa uchaguzi Mkuu uliopagwa kufanyika mwezi Mei, 2024.
Hatua hii imekuja baada ya Zuma kukata rufaa, akipinga kuzuiwa na Tume ya Uchaguzi kuwania wadhifa wowote kwenye uchaguzi huo kutokana na rekodi ya kuhukumiwa na kufungwa jela kwa zaidi ya miezi 12.
Uamuzi huu ni muhimu kwa Zuma mwenye umri wa miaka 81, ambaye baada ya kusimamishwa kwenye chama tawala cha ANC, alihamia chama kipya cha upinzani cha uMkhonto we Sizwe.