Katika kuhakikisha usalama barabarani unaimarika, ukurasa wa Mabalozi wa Usalama Barabarani Nchini – RSA, umechapisha andiko la matukizi ya Indiketa katika mzunguko wa Barabara ya mzunguko (Round about).

RSA inahikiza mtumiaji wa barabara kujitahidi kuzingatia matumizi ya indiketa kwenye eneo hilo kwa kusema kitu cha kwanza ni mtumiaji huyo kutakiwa kupunguza Mwendo.

Aidha, wanaelimisha kuwa mtumiaji wa barabara kitu cha pili anatakiwa kuangalia alama na ishara zote zilizopo katika mzunguko na kitu cha tatu ni kufanya maamuzi ya mapema ni njia gani anataka kutumia iwapi ni ya kushoto ama ya kulia.

Jambo la nne ni kama mtumiaji wa barabara atafika kwenye mzunguko na nia yake sio kuzunguka bali kutokea kushoto mwa mzunguko, basi aoneshe indiketa kumuashiria dereva mwingine kuwa hutazunguka badala yake anatoka kwa kutumia filta iliyopo kushoto kwake.

Iwapo mtumiaji wa barabara atakuwa anaingia kwenye mzunguko na lengo lake ni kuzunguka, basi ni vizuri kutumia indiketa ya kulia kuonesha anazunguka, na atakapokuwa anatoka pia ataonesha indiketa ya kushoto kama ishara, hili ni jambo la tano.

Jambo la sita unapoingia kwenye mzunguko wakati wote toa kipaumbele kwa magari yanayozunguka mzunguko na saba ahakikishe anasimama kwenye zebra zilizo karibu na mzunguko, ili kuwapisha waenda kwa miguu, kama wapo.

RSA inaeleza kuwa, kwa namna hii ni wazi kuwa mtumiaji wa barabara ataepusha ajali ndogo ndogo au kadhia inayoweza kutokea kwenye mzunguko wakati wa kuingia ama kutoka, kwani mzunguko unasaidia kupunguza ajali kwa asilimia 80.

Faye amtaka Sonko kuimarisha uchumi, sekta ya fedha
Urais: Mahakama yamuondolea Zuma vizuizi