Joto kali na unyevu mara nyingi husababisha kupoteza hamu ya kula, hivyo ni muhimu kula mara kwa mara ili kuupa mwili wako virutubisho sahihi ili kukabiliana na joto na kuwa na afya njema, kwa kudumisha lishe bora na kunywa maji mengi kitu ambacho ni muhimu katika kulainisha mwili na ngozi.
Hapa nakuletea orodha ya baadhi ya vyakula ambavyo si tu vinaburudisha kula wakati wa joto la kiangazi bali vina afya kwa ajili ya mwili wako na ndivyo sahihi wakati wa majira ya joto.
TANGO: Hukupatia maji mara moja na kupunguza joto la mwili. unaweza kula tango kama saladi au kama juisi kukuburudisha.
TIKITI: Tikiti maji limejaa virutubishi muhimu. Hutia mwili unyevu na lina Vitamini B, Magnesiamu, Potasiamu na Nyuzinyuzi.
MTINDI: Kinywaji ambacho kina manufaa kwa usagaji na usagaji chakula. unaweza kuongeza ladha yake na mbegu za cumin iliyochomwa.
EMBE: Tunda hili lenye matumizi mengi husaidia usagaji chakula, hupoza mwili na kuongeza viwango vya nishati.
MTINDI WA KUCHEKECHA: Wanaita Yghurt, wenyewe una kalsiamu na bakteria zinazofaa kwa utumbo, ni mbadala wa majira ya kiangazi. Changanya na embe, ufurahie.
SAMAKI: Hili ni chaguo lililojaa protini ambalo hutoa joto la ndani kidogo kuliko nyama. Unaweza kufurahia faida za asidi nzuri ya mafuta bila kujisikia kushiba.
PARACHICHI: Ina asidi ya mafuta ambayo husaidia kuondoa joto na sumu mwilini, parachichi humeng’enywa kwa urahisi na kuuepusha mwili wako na uzalishaji wa joto kupita kiasi.
NAZI: Yenyewe imejazwa elektroliti, maji ya nazi huhifadhi unyevu na baridi. Yana utajiri wa virutubisho muhimu kwa nishati na uwezo wa usagaji chakula.
MINT: Inapunguza athari za joto na ina hisia ya baridi. Mint ni nzuri katika vinywaji au huongezwa kwa saladi ili kuburudisha.
LIMAO: Huimarisha mfumo wa kinga kwa kutumia kipimo cha kiafya cha Vitamini C. Ifurahie kama limao au ongeza kipande kidogo kwenye juisi na saladi, ili kukuburudisha.