Mwakilishi wa Familia ya aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Edward Sokoine, Balozi Joseph Sokoine Mfumo wa maji uliopo katika vijiji vya Wilaya ya Monduli mkoani Arusha ni wa miaka ya 1970 wakati vijiji hivyo vikiwa na watu wachache hivyo upatikanaji wa maji haukidhi mahitaji.
Balozi Joseph Sokoine ameyasema hayo hii leo Aprili 12, 2024 mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan katika maadhimisho ya miaka 40 ya kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania, Hayati Edward Sokoine.
Amesema, “tunashukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutusaidia kutatua changamoto ya maji safi na salama kwani tuna imani kuwa mradi wa maji unaotoka Arusha kuja kwetu kijijini Monduli utamaliza uhaba wa maji,” Balozi Sokoine amemweleza Rais Samia.
Naye, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda amearifu kuwa Rais Samia amekusudia kujenga barabara ya lami yenye urefu wa kilomita 11.66 kutoka Ngareshi hadi Monduli Juu ambapo Hayati Sokoine amezaliwa, huku Rais Samia akisema watu wengi hawamjui Hayati Edward Sokoine hivyo Serikali itamuenzi kwa kufanya kazi kwa weledi.
Rais Samia amesema Watanzania wanne kati ya watano hawana kumbukumbu zao wenyewe wala hawakuishi kuona uongozi wa Sokoine.