Boniface Gideon, Pangani – Tanga.
Kufuatia kilio cha siku 23 cha kukosekana kwa huduma za uvushaji abiria na mizigo katika Kivuko cha MV. Pangani Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tanga kimeijia juu Mamlaka inayosimamia Kivuko hicho ‘Wakala wa ufundi na umeme Serikalini TEMESA’ kwakutoa maagizo mazito na hatua za haraka ambazo zitasaidia kurudisha mawasiliano ya Wilaya hiyo iliyogawanyika pande mbili kupitia Mto Pangani ambao umeungana na Bahari.
Katika ziara iliyofanyika hii leo Aprili 22, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga, Rajab Abdallarrham ameitaka TEMESA kuhakikisha wanafanya matengenezo hayo haraka huku akiitaka Mamlaka hiyo kuchukua hatua za kusimamia uvushaji abiria na mizigo kwakutumia Mitumbwi na Boti ili kuongeza Usalama kwa Wananchi.
Amesema Wakazi wa Wilaya hiyo pamoja na Wafanyabiashara wamekuwa wakiteseka kwa zaidi ya wiki tatu na kwamba, “takribani mwezi sasa huduma za uvushaji abiria na mizigo kwakutumia Kivuko hiki hakifanyi kazi, Wananchi wetu wanateseka sana kuvuka hapa, wanitumia Mitumbwi kitu ambacho ni hatari kwa Afya zao,ni lazima Mamlaka husika ichukue hatua za haraka, lakini pia kwa Wananchi ambao hawana ulazima wa kuvuka ni vizuri mkaacha kuvuka ni hatari kwa kufanya hivyo.”
Akitoa Majibu ya kadhia hiyo, Msimamizi wa Wakala wa ufundi na umeme Serikalini TEMESA Kanda ya Mashariki na kusini, Mhandisi Lukombe King’ombe amesema tatizo la kuharibika kwa kwakivuko hicho lilianza wiki tatu zilizopita huku changamoto kubwa ni uchakavu wa mitambo nakwamba huduma hiyo itarejea wakati wowote kuanzia sasa nakwamba huduma za uvushaji abiria na mizigo zitarejea wakati wowote kuanzia sasa.
“Tuliagiza vipuli nje ya Nchi na vimeshawasili tayari, huduma hii itarejea kwenye hali yake kama kawaida,hapa tuna vivuko viwili lakini kimoja kinahitaji matengenezo Makubwa lakini pia kinachangamoto za kisera na sio utendaji ikiwemo kuwa na Bima pamoja na Leseni, kwahiyo niwatoe hofu wadau wote wanaotumia Kivuko hiki kuwa huduma zitarejea wakati wowote kuanzia sasa,” alisema King’ombe