Katika kuelekea kwenye maadhimisho ya Miaka ya 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, inatarajia kuajiri Walimu wapya wa masomo ya Sayansi na kuendelea kuboresha maslahi yao.

Hayo yamebainishwa hii leo Aprili 22, 2024 na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi wakati akifungua Skuli ya ghorofa ya Sekondari Hassan Khamis Hafidh iliyopo Monduli, Wilaya ya Magharibi A , Mkoa wa Mjini Magharibi.

Amesema, ujenzi wa miundombinu ya Skuli ina lengo la kuboresha ili kupunguza msongamano wa wanafunzi na kutozidi idadi ya 45 kila darasa, huku akiipongeza Wizara ya Elimu kwa kazi nzuri ya kuvuka malengo ya ilani ya utekelezaji ya uchaguzi ya CCM 2020-2025.

Rais Dkt. Mwinyi pia amewataka wananchi kuendelea kuudumisha Muungano, ili kupata maendeleo katika nyanja zote za Afya, Elimu kiuchumi.

CCM yaibana TEMESA huduma za MV. Pangani kushindikana
Liverpool kuivurugia Man Utd kwa Mikayil Faye