Wakala wa misitu Tanzania – TFS, Wilaya ya Rufiji umekabidhi mizinga ya nyuki ya kisasa 300 kwa Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Serikali za mitaa TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa kwa ajili ya Vikundi 38 vya Vijana vilivyoomba msaada huo.

Alikabidhi mizinga hiyo kwa niaba ya Kamishina Muhifadhi TFS, Prof. Do santos Silayo Ikwiriri Wilayani Rufiji Mkoani Pwani, Meneja wa TFS Wilaya ya Rufiji, Francis Kiondo alisema itawasaidia Vijana hao katika kujiimarisha kiuchumi.

Alisema, vikundi vitatu vitakabidhiwa kwa niaba ya vikundi vingine ambapo kila kimoja kitapata mizinga ya nyuki ya kisasa kumi, ambayo ina uwezo wa kutoa mpaka kilo 20 za asali kwa mwaka, huku alivitaja vikundi vitatu vilivyokabidhiwa kuwa ni pamoja na Chama Cha ushirika wa Vijana Wajasiriamali, Ikwiriri shotern karate na kikundi cha UVCCM kwa Mpalange.

Akipokea Mizinga hiyo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mohamed Mchengerwa ameishukuru Wizara ya Maliasili na TFS kwa ushirikiano hasa katika kipindi hiki cha mafuriko ya Mto Rufiji ikiwa ni pamoja na Msaada wa Boti, Vyakula na Maturubai.

De Bruyne afichua siri ya maisha Man City
Wajumbe wa bodi wamkataa Ten Hag