Kiungo kutoka nchini Ubelgiji Kevin De Bruyne amekiri kujivuniua kuwa sehemu ya kikosi cha kwanza cha Mabingwa Watetezi wa Ligi Kuu ya England Manchester City.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 32, alimwagiwa sifa kede kede na wachezaji wenzake wa Manchester City kufuatia kiwango safi alichokionesha kwenye Nusu Fainali ya Kombe la FA dhidi ya Chelsea iliyokubali kufungwa 1-0, mwishoni mwa juma lililopita.

Bao la Kiungo kutoka nchini Ureno Bernardo Silva lilitosha kuizuia Chelsea kutinga Fainali ya Kombe la FA msimu huu 2023/24, ambapo watacheza na Manchester United.

De Bruyne amesema amekuwa akijihisi furaha na faraja kwa kuendelea kuwa sehemu ya kikosi cha kwanza cha Manchester City, ambacho kimekuwa na mafanikio msimu hadi msimu.

Amesema asilimia kubwa ya mafanikio yake yanatokana na ushirikiano na upendo uliotawala miongoni mwa wachezaji wa klabu hiyo, hivyo hilo linaendelea kumpa faraja na kujiona ni mwenye mafanikio.

“Jinsi tulivyofanya mwaka mzima imekuwa nzuri,” amesema De Bruyne kuhusu uwezo na tabia ya timu yake, siku chache baada ya kutolewa kwenye Ligi ya Mabingwa katika hatua ya Robo Fainali na Real Madrid.

“Mwaka jana na tulikuwa tunacheza kwenye michuano ya aina tatu, sasa tunashiriki kwenye michuano miwili, lakini kufanya hivi mwaka baada ya mwaka ni ishara ya tabia ya timu yetu kufanya vizuri.

“Ninajivunia na ni heshima kucheza kwenye timu hii kwa sababu tunaonesha kuhitaji kitu cha mafanikio kila msimu.”

“Nina furaha sana. Mchezo wetu dhidi ya Chelsea ulikuwa mchezo mgumu, na tulijitoa kwa asilimia 100, ndio maana tulifanikiwa kushinda, na hilo linaendelea kunipa faraja na kujihisi fahari kuwa sehemu ya kikosi cha Man City” ameongeza

“Tupambana, tulifanya kazi kwa bidii na tukapata njia ya kushinda. Tulifanya utendakazi kazi bora tulioweza kufanya, tulikuwa tumechoka baada ya mchezo wetu wa Jumatano dhidi ya PSG, lakini tulifanya hivyo na kurudi kwenye Fainali ya Kombela FA, nadhani ni ishara nzuri ya tabia.

“Jinsi tulivyocheza dhidi ya Real Madrid ilikuwa nzuri sana na Jumamosi tulicheza kwa huzuni kidogo baada ya Jumatano, lakini tuna furaha tunaweza kurejea Fainali.” amesema kiungo huyo

Dkt. Mpango: Watanzania wanahitaji kufanya kazi kwa bidii
TFS wapeleka tumaini jipya la Vijana kiuchumi Rufiji